KATIBU Mkuu wa CECAFA, Nicholaus Musonye ametangza ratiba ya michuano ya Kombe la Kagame itakayoanza kutimua vumbi Julai 18, 2015 jijini Dar es salaam ikishirikisha timu 13 kutoka nchi wanachama wa CECAFA. Mechi ya ufunguzi tarehe 18 Julai, 2015 Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam itashuhudia wenyeji Yanga SC wakicheza na Gor Mahia ya Kenya, huku APR ya Rwanda ikicheza na Al Shandy ya Sudan na KMKM ya Zanzibar wakifungua dimba na Telecom ya Somalia. Ratiba ya michuano hiyo imeziweka timu hizo katika makundi matatu ambapo kundi A lina timu za: Yanga (Tanzania), Gor Mahia (Kenya), Telecom (Djbiout), KMKM (Zanzibar) na Khartoum-N (Sudan) Kundi B: APR (Rwanda), Al Shandy (Sudan), LLB AFC (Burundi) na Heegan FC (Somalia), Kundi C: Azam FC (Tanzania), Malakia (Sudan Kusini), Adama City (Ethiopia) na KCCA (Uganda). Timu tatu zitakazoshika nafasi ya juu kutoka kundi A, timu mbili za juu kutoka kundi B & C, na mshindi mwenye wastani mzuri kutoka kundi B & C zitaingia katika hatua ya robo fainali.
Wednesday, July 1, 2015
CECAFA YATOA RATIBA YA KAGAME 2015.

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment