TIMU ya taifa ya Uingereza imeaga michuano ya Kombe la Dunia kwa wanawake kwa majonzi baada ya bao la kujifunga wenyewe la Laura Basset kuwavusha mabingwa watetezi Japan katika hatua ya fainali. Uingereza walikuwa wakijaribu kutinga fainali ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza huku wakitaraji kuwa timu ya pili nchini humo kufanya hivyo baada ya timu ya wanaume kunyakuwa taji hilo mwaka 1996. Katika mchezo huo Uingereza walionyesha jitihada zao za kuweka kuupeleka mchezo katika muda wa nyongeza lakini bao la kujifunga la Basset katika dakika za majeruhi zilikwamisha ndoto yao hiyo. Japan sasa wanajiandaa kucheza na Marekani katika mchezo wa fainali utaofanyika jijini Vancouver Jumapili hii, mchezo ambao utakuwa kama marudio ya fainali kati ya timu hizo iliyofanyika mwaka 2011 ambapo Japan waliibuka kidedea kwa changamoto ya mikwaju ya penati. Kwa upande wa Uingereza wao sasa wanatarajia kucheza na Ujerumani Jumamosi hii kutafuta nafasi ya mshindi wa tatu.
No comments:
Post a Comment