KLABU ya Bayern Munich inatarajiwa kuanza ziara yake ya maandalizi ya msimu mpya wa Bundesliga bila kuwa na nyota wake Arjen Robben ambaye amelazimika kujitoa kutokana na majeruhi. Winga huyo mwenye umri wa miaka 31, alijumuishwa katika kikosi kitakachofanya ziara yake nchini China, lakini sasa atabakia nyumbani kwa tahadhari baada ya kupata matatizo ya msuli. Robben alikosa sehemu kubwa ya mzunguko wa pili wa Bundeslga msimu uliopita na Bayern haina mpango ya kuhatarisha afya yake kuelekea katika msimu mpya. Franck Ribery, Holger Badstuber, Dante na Jan Kirchhoff nao pia wameachwa kutokana na kutokuwa fiti kwa asilimia 100. Bayern wanatarajia kuzuru miji ya Peking, Shanghai na Guangzhou katika kipindi cha siku nane watakachokuwa China huku wakicheza mechi za kirafiki na Valencia Jumamosi hii, Inter Milan Jumanne ijayo kabla ya kuvaana na wenyeji Guangzhou Evergrande katika mchezo wa mwisho utakaochezwa Julai 23.
No comments:
Post a Comment