MSHAMBULIAJI wa zamani wa klabu za Real Madrid na Manchester City, Robinho amejiunga na klabu ya Guangzou Evergrande ya China. Nyota huyo wa kimataifa wa Brazil ambaye alicheza katika michuano ya Copa America, amesaini mkataba wa miezi sita kuitumikia timu hiyo. Uhamisho huo unamfanya nyota huyo mwenye umri wa miaka 31, kuungana na kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil Luiz Felipe Scolari pamoja na mchezaji mwenzake Paulinho. Paulinho ambaye ni kiungo wa zamani wa klabu ya Tottenham Hotspurs alijiunga na Guangzhou mwishoni mwa mwezi uliopita na tayari ameshaichezea timu hiyo mechi mbili. Robinho ambaye atakuwa akivaa jezi yenye namba 60, amewahi kuichezea City mechi 53 kati ya mwaka 2008 na 2010 baada ya kujiunga timu hiyo kwa kitita cha paundi milioni 32.5 akitokea Madrid.
No comments:
Post a Comment