Friday, July 3, 2015

CHELSEA YAMCHUKUA RASMI FALCAO KWA MKOPO.

KLABU ya Chelsea imefanikiwa kumsajili mshambuliaji wa Monaco Radamel Falcao kwa mkopo wa msimu mzima huku kukiwa na uwezekano wa kumchukua moja kwa moja. Nyota huyo wa kimataifa wa Colombia msimu uliopita alikuwa kwa mkopo Manchester United lakini mambo hayakumuendea vyema sana baada ya kufunga mabao manne katika mechi 29 alizocheza. Falcao sasa anaungana na wachezaji wenzake wa zamani wa Atletico Madrid Thibaut Courtois, Filipe Luis na Diego Costa. Kiungo wa kimataifa wa Croatia Mario Pasalic mwenye umri wa miaka 20 yeye anakwenda Monaco kwa mkopo akipishana na Falcao. Falcao alifunga mabao 72 katika misimu miwili aliyoichezea FC Porto kuanzia mwaka 2009 mpaka 2011 kabla ya kujiunga na Atletico Madrid ambako nako aliendelea wimbi hilohilo kwa kufunga mabao 70 katika misimu miwili pia na kunyakuliwa na Monaco mwaka 2013 kwa kitita cha paundi milioni 50.

No comments:

Post a Comment