KLABU ya Chelsea inabidi isubiri kutuma ofa yake kwa ajili ya kumuwania Pedro mpaka baada ya uchaguzi wa Barcelona Julai 18 mwaka huu kwasababu uongozi wa muda wa klabu hiyo umezuiwa kufanya maamuzi yeyote kuhusiana na usajili. Meneja wa Chelsea amekuwa akimtaka winga huyo mwenye umri wa miaka 27 ambaye anakadiriwa kufikia thamani ya paundi milioni 22 na uamuzi wa kumuuza au kumuacha abaki utafanywa na rais mpya atakaechaguliwa kuingoza Barcelona. Tayari Ramon Adell ambaye ni kiongozi wa muda ameshakosolewa vikali na wagombea nafasi ya urais katika uchaguzi huo kwa kumsajili Arda Turan kutoka klabu ya Atletico Madrid. Chelsea wana matumaini makubwa ya kumnasa Pedro kutokana na nafasi yake katika kikosi cha Barcelona kuzidi kuwa finyu kutokana na ujio wa Luis Suarez kiangazi mwaka jana. Kama akijiunga na Chelsea atakuwa pamoja na mchezaji mwenzake wa zamani Cesc Fabregas pamoja na wachezaji wengine ambao wanaongea lugha ya Hispania Diego Costa, Cesar Azpilicueta na Felipe Luis.
No comments:
Post a Comment