KIBARUA cha Robin van Persie katika klabu ya Manchester United kinakaribia ukingoni baada ya mshambuliaji huyo kutua nchini Uturuki tayari kumalizia hatua za mwisho za uhamisho wake kwenda Fenerbahce. Van Persie alionekana akiwa na tabasamu pana pindi alipotua katika Uwanja wa wa Ndege wa Sabhia Gokcen uliopo jijini Instabul jana mchana. Nyota huyo wa kimataifa wa Uholanzi alipokewa kwa shangwe na bashasha na mashabiki wa Fenerbahce waliojitokeza uwanjani hapo kumlaki jembe lao jipya. Mapema jana, Van Persie alituma picha katika mitandao ya kijamii ikimuonyesha yeye pamoja na familia yake nje ya ndege binafsi ambayo ndio alioitumikia kutoka Uwanja wa Ndege wa Manchester mpaka Instabul. Van Persie ambaye tayari ameshafaulu vipimo vya afya alivyofanyiwa mapema leo, anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka mitatu na klabu hiyo ambao utamuwezesha kulipwa kitita cha paundi 240,000 kwa wiki.
No comments:
Post a Comment