Monday, July 6, 2015

CITY YANASA KINDA LA UTURUKI.

KLABU ya Manchester City imemsajili mshambuliaji chipukizi wa kimataifa wa Uturuki mwenye umri wa miaka 18 Enes Unal kutokea klabu ya Bursaspor kwa ada ambayo haikuwekwa wazi. Unal ambaye ameichezea timu yake ya taifa mara moja, amefunga mabao manne katika mechi 37 za Ligi Kuu ya Uturuki alizoichezea Bursaspor na kuisaidia kushika nafasi ya sita msimu uliopita. Aliitwa kwa mara ya kwanza kuitumikia timu ya wakubwa ya Uturuki Machi mwaka huu katika mchezo dhidi ya Luxembourg baada ya kufunga mabao 24 katika mechi 25 alizochezea timu ya vijana chini ya umri wa miaka 16. Mwaka 2013 akiwa na umri wa miaka 16, aliweka historia kwa kuwa mchezaji mdogo zaidi kufunga bao katika Ligi Kuu ya nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment