KIUNGO wa klabu ya Tottenham Hotspurs, Nabil Bentaleb amesaini mkataba mpya wa miaka mitano ambao utamuweka White Hart Lane mpaka mwaka 2020. Mazungumzo ya mkataba mpya yalionekana kama kukwama msimu uliopita huku nyota huyo wa kimataifa wa Algeria akieleza kukerwa kwake na kuchelewa kwa makubaliano lakini sasa hatimaye wameshalimaliza hilo. Akihojiwa mapema Juni, Bentaleb amesema amekuwa akifanya kazi kwa bidii na hivyo ni haki yake kuhitaji kuthaminiwa kwa mchango wake huo. Mara baada ya kusaini mkataba huo nyota huyo aliwshukuru wale wote waliofanikisha hilo kwani amekuwa akibidiika ili kupata mkataba wa aina hiyo.
No comments:
Post a Comment