Monday, July 6, 2015

OFISA WA FIFA AFUNGIWA MIAKA SABA.

OFISA w Shirikisho la Soka Duniani-FIFA ambaye alikuwa akitathmini zabuni zilizotolewa kwa ajili ya uenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 na 2022 amefungiwa kujishughulisha na masuala yeyote ya soka kwa muda wa miaka saba. Ofisa huyo Harold Mayne-Nicholls mwenye umri wa miaka 54 amefungiwa na kamati ya maadili ya shirikisho hilo. Katika taarifa yake FIFA imedai kuwa taarifa zaidi kuhusiana na hilo zitatolewa wakati uamuzi huo utakapoanza kufanya kazi. Mayne-Nicholls amepanga kukata rufani kupinga adhabu hiyo na kuhoji kwanini imetangazwa kabla hajamaliza taratibu za rufani. Mayne-Nicholls ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa kundi la kutathmini zabuni za Kombe la Dunia mwaka 2018 na 2022 ambapo nchi za Urusi na Qatar ndio zilishinda.

No comments:

Post a Comment