Saturday, July 18, 2015

DELPH ASAINI MIAKA MITANO CITY.

NAHODHA wa Aston Villa Fabian Delph amesaini mkataba wa miaka mitano katika klabu ya Manchester City ikiwa imepita wiki moja baada ya kudai atabakia Villa Park. Kiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza, uhamisho wake kwenda City umekuja baada ya kueleza msimamo wake kuhusu mustakabali wake. Akihojiwa meneja wa City, Manuel Pellegrini amesema Delph ambaye ana umri wa miaka 25 bado ana miaka mingi ya kucheza soka kwa kiwango cha juu hivyo ana hamu kubwa ya kufanya naye kazi. Delph alikamilisha vipimo vya afya jana na anatarajiwa kusafiri leo kuelekea nchini Australia kujiunga na wachezaji wenzake kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu. Nyota huyo amepewa jezi namba nane ambayo ilikuwa ikitumiwa na Frank Lampard msimu uliopita ambaye kwasasa yuko katika klabu ya New York City FC ya Marekani.

No comments:

Post a Comment