Saturday, July 18, 2015

MCHEZAJI WA ZAMANI WA ARSENAL ALIMWA KADI BAADA YA KUWAJIBU WALIOMFANYIA VITENDO VYA KIBAGUZI.

MCHEZAJI wa zamani wa Arsenal, Emmanuel Frimpong alijikuta akitolewa nje akiwa na timu yake ya FC Ufa ya Urusi baada ya kuonyesha ishara ya tusi akijibu mashabiki waliokuwa wakimpigia kelele za nyani. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23, alikuwa kicheza ugenini dhidi ya Spartak Moscow katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu ya nchi hiyo. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo ambao ulimalizika kwa sare ya mabao 2-2, nyota huyo wa kimataifa wa Ghana amesema wakati mchezo uliposimama mashabiki walianza kumpigia kelele za nyani. Frimpong aliendelea kudai kuwa alishindwa kuzua jazba zake na kuonyesha hisia zake na hilo ndilo kosa lilofanya. Frimpong alionyeshwa kadi nyekundu baada ya nusu ya mchezo huo wakati ambapo timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1.

No comments:

Post a Comment