Thursday, July 23, 2015

HOFU YAMUINGIA WENGER AKIWAZA KUSTAAFU.

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amesema mawazo ya kustaafu humfanya kuingiwa na hofu. Meneja huyo raia wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 65, anatarajiwa kutimiza miaka 20 akiwa na Arsenal lakini amesema hana mpango wowote wa kufuata nyayo za meneja wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson aliyestaafu. Akihojiwa kuhusiana na hilo, Wenger amesema huwa analiwaza kwa muda usiozidi sekunde tano kwasababu humfanya apate hofu kidogo. Wenger aliendelea kudai kuwa wakati walipocheza na United alikutana na Ferguson na kumuuliza kama haoni kama kuna kitu anakikosa lakini alimjibu kuwa alishafanya ikamtosha kabisa. Wenger ambaye ameiongoza Arsenal kutetea taji lake la FA msimu uliopita, aliongeza kuwa pamoja na hayo lakini ni mara chache sana kumkosa Ferguson uwanjani. Wenger alijiunga na Arsenal akitokea Monaco mwaka 1996.

No comments:

Post a Comment