Thursday, July 23, 2015

MOURINHO AMKINGIA KIFUA GOLIKIPA WAKE GARASA ALIYEMCHUKUA KUTOKA STOKE.

MENEJA wa Chelsea, Jose Mourinho amemkingia kifua golikipa mpya Asmir Begovic baada ya nyota huyo wa kimataifa wa Bosnia kuruhusu mabao manne katika mchezo dhidi ya New York Redbull kufuatia kuingia kwake wakati wa mapumziko katika mchezo huo wa kirafiki uliochezwa jana. Begovic alisajiliwa akitokea Stoke City mwezi huu kwa akitita cha paundi milioni nane ili aweze kuleta changamoto kwa golikipa namba moja Thibaut Courtois. Katika mchezo huo Begovic alibadilishana na na Courtois Chelsea wakiwa wanaongoza kwa bao 1-0 lakini mambo yalibadilika na kujikuta wakichapwa mabao 4-2. Akihojiwa Mourinho amesema Begovic alikuwa amechoka kama ilivyokuwa kwa Courtois na golikipa akichoka siku zote huwa kunakosekana kwa uelewano. Mourinho aliendelea kudai kuwa Courtois alifanya makosa katika kipindi cha kwanza na Begovic naye alifanya makosa katika kipindi cha pili kwa kukosa kasi katika matukio jambo ambalo ni matokeo ya uchovu unaotokana na mazoezi makali.

No comments:

Post a Comment