Thursday, July 16, 2015

LAMPARD, PIRLO HAWAJAENDA MAREKANI KWASABABU YA FEDHA.

MKURUGENZI wa michezo wa klabu ya New York City, Claudio Reyna amedai kuwa Frank Lampard na Andrea Pirlo hawajajiunga na timu hiyo kwasababu ya pesa. Pirlo ambaye ni kiungo wa zamani wa Juventus analipwa kitita cha paundi milioni 5.17 kwa mwaka na kumfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi katika Ligi Kuu ya Soka ya Marekani-MLS, wakati Lampard yeye anakunja kitita cha paundi milioni 3.8 kwa mwaka. Akihojiwa Reyna amesema aliwauliza swali hilo kwanini haswa wamekuja MLS na jibu walilotoa lilikuwa ni kwa ajili ya kushindana na sio pesa. Lampard alikosa mchezo wa Jumapili iliyopita ambapo timu yake ilitoka sare ya mabao 4-4 dhidi ya Toronto FC kutokana na majeruhi. Pirlo ambaye anataka kuwa sehemu ya kikosi cha Italia kitakachoshiriki michuano ya Ulaya mwaka 2016 anaweza kuanza kuitumikia kwa mara ya kwanza timu hiyo wakati itakapochuana na Orlando katika Uwanja wa Yankee Julai 26 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment