SHIRIKISHO la Soka la Nigeria, limeteua kiungo na nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya nchi hiyo Sunday Oliseh kuwa kocha mpya. Oliseh mwenye umri wa miaka 40 amesaini mkataba wa miaka mitatu akichukua nafasi ya Stephen Keshi aliyetimuliwa mapema mwezi huu. Akihojiwa Oliseh amesema wana vipaji vya kubadilisha muelekeo, kurejesha heshima na kupata matokeo yanayostahili. Nguli huyo wa zamani aliendelea kudai kuwa kazi hiyo ni kubwa katika soka la Afrika na akipata ushirikiano wa kutosha hana shaka kuwa watarejesha heshima ya Super Eagles kama ilivyokuwa mwanzoni. Oliseh amewahi kuitumikia kuichezea Super Eagles mehi 63 na kuisaidia kunyakuwa taji la michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka 1994 na medali ya dhahabu katika michuano ya olimpiki mwaka 1996.
No comments:
Post a Comment