BINGWA wa dunia wa uzito wa welter, Floyd Mayweather amevuliwa mkanda wake wa dunia wa WBO ambao alishinda kwa kumpiga Manny Pacquiao Mei mwaka huu. Bondia huyo mwenye umri wa miaka 38 amevuliwa ubingwa huo baada ya kushindwa kulipa ada ya paundi 128,000 ambayo muda wake wa mwisho ulikuwa Julai 3 mwaka huu. Mayweather alitegemewa kuachia mkanda huo baada ya kudai kuwa alipanga kufanya hivyo kufuatia ushindi wake wa alama aliopata dhidi ya Pacquiao. Baada ya kumchapa Pacquiao, Mayweather alibainisha kuwa ataachia mikanda yake yote ili kutoa fursa kwa mabondia chipukizi kugombania. Mayweather bado anashikilia mikanda ya WBA na WBC na amepewa mpaka Julai 20 ili kuukatia rufani uamuzi huo.
No comments:
Post a Comment