TIMU ya taifa ya Micronesia imepokea kipigo kingine cha kudhalilisha kwa kutandikwa mabao 46-0 na Vanuati na sasa taifa hilo la bara la Pacific limeiangukia Shirikisho la Soka la Duniani-FIFA wawasaidie kuimarika. Kabla ya mchezo huo Micronesia tayari walikuwa wameshatandikwa mabao 38-0 na Fiji na mengine 30-0 na Tahiti katika michuano hiyo bara hilo hivyo kumaanisha kutandikwa jumla ya mabao 114 katika mechi zao tatu za makundi. Kocha wa Micronesia Stan Foster ambaye ni raia wa Australia amekiri mchezo huo uloikuwa kati ya wavulana na wanaume waliokamilika na kuwataka maofisa wa FIFA kulitambua taifa hilo kwa kuliingiza katika viwango vya ubora. Kocha huyo amesema FIFA wakifanya hivyo kutafungua milango ya kupata misaada ya kiufundi ambayo itaweza kuwasaidia kujiimarisha zaidi.
No comments:
Post a Comment