Wednesday, July 8, 2015

MILAN YAKUBALIWA KUPEWA ENEO KWA AJILI YA KUJENGA UWANJA WAO MPYA.

KLABU ya AC Milan imepiga hatua moja kubwa katika mipango yake ya kujenga uwanja mpya baada ya ombi kukubaliwa na mfuko unaomiliki ardhi ya eneo wanalotaka kujenga. Milan ambao kwasasa wanatumia kwa pamoja Uwanja wa San Siro na mahasimu wao Inter Milan, wamepanga kujenga uwanja mpya wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 48,000 mpaka kufika msimu wa 2018-2019. Mkurugenzi wa klabu hiyo Barbara Berlusconi amesema hiyo ni hatua ya kihistoria kwani ndio mwanzo wa kuelekea katika malengo waliyojiwekea ya kuwa na uwanja wao wenyewe. Barbara ambaye ni binti wa mmliki wa klabu hiyo Silvio Berlusconi, ametabiri kuwa uwanja huo utaweza kuwaingizia kati ya euro milioni 50 na 80 kwa mwaka yakiwa kama mapato ya ziada.

No comments:

Post a Comment