KIUNGO mpya wa Barcelona, Arda Turan amesema itamuwia vigumu kwake kutoweza kupata nafasi ya kucheza mpaka Januari kufuatia adhabu iliyopewa timu hiyo na Shirikisho la Soka Dunia-FIFA. Barcelona ilikubali kumsajili nahodha huyo wa Uturuki kutoka Atletico Madrid Juzi na vyombo vya habari vya Hispania kudai kuwa mabingwa hao wa Ulaya wanaweza kumpeleka kwa mkopo mpaka mwakani huku klabu ya Galatasaray ikitajwa. FIFA iliifungia Barcelona kutosajili kwa misimu miwili baada ya kukutwa na hatia ya kusajili wachezaji walio na umri chini ya miaka 18 kinyume na sheria zake. Akihojiwa Turan amesema anajua itakuwa vigumu kutoweza kucheza kwa muda miezi sita lakini jambo la muhimu ni kuwa ataichezea Barcelona wakati ukifika. Kiungo huyo aliendelea kudai kwa wakati huu atakuwa akijifua kwa ajili ya kuja kuitumikia klabu yake hiyo mpya na kuisaidia kushinda mataji zaidi. Turan mwenye umri wa miaka 28, pia anahusishwa na taarifa za kutakiwa kwa mkopo Fenerbahce.
No comments:
Post a Comment