Friday, July 3, 2015

MKONGWE TOMMASI AREJEA TENA UWANJANI BAADA YA KUSTAAFU.

KIUNGO wa zamani wa Italia, Damiano Tommasi amereje tena uwanjani akiwa na umri wa miaka 41 baada ya kustaafu akiichezea timu ya La Fiorita ya San Marino katika mchezo wa michuano ya Europa League dhidi ya FC Vaduz jana. Tommasi ambaye alitundika daruga zake miaka sita iliyopita na akiwa rais wa Chama cha Wacheza Soka nchini Italia, alicheza kwa dakika 90 kwenye mchezo huo ingawa alishindwa kuzuia timu yake kuchabangwa mabao 5-0. Wiki iliyopita Tommasi alidai kuwa anataka watoto wake wapate nafasi ya kumuona akicheza mashindano ya kimataifa huku akitaka kungeza ukurasa mwingine katika kipindi chake cha uchezaji soka. Tommasi amefuata nyayo za beki wa kimataifa wa Brazil, Aldair mchezaji mwingine wa AS Roma ambaye alirejea tena uwanjani baada ya kustaafu ya kuichezea klabu ya SS Murata katika michuano ya kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2007 na 2008 akiwa namiaka 40.

No comments:

Post a Comment