MENEJA wa Manchester City amepongeza ujio wa Raheem Sterling katika kikosi chake na kusisitiza winga huyo wa kimataifa wa Uingereza aliyesajiliwa kwa kitita cha paundi milioni 49 anastahili thamani hiyo. Baada ya kukamilisha usajili wake kutoka Liverpool Jumanne iliyopita, Sterling alikwea pipa kwenda kujiunga na kikosi cha Manchester City kilichokuwa katika ziara ya maandalizi ya msimu mpya. Sterling aliwaji jijini Brisbane, Australia jana usiku kabla ya kuanza mazoezi rasmi ka mara ya kwanza mapema leo. Nahodha a City Vicente Kompany ameshaweka wazi kuwa Sterling atakaribishwa katika kikosi chao kwa mikono miwili ambapo nyota huyo alionekana akitabasamu muda wa mazoezi ya timu hiyo na wachezaji wenzake akiwemo David Silva. Pellegrini alithibitisha Sterling hatakuwepo katika kikosi kitakachocheza mchezo wa kirafiki kesho dhidi ya Melbourne City ambayo pia inamilikiwa na klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment