MENEJA wa Manchester City, Manuel Pellegrini amesaini mkataba mpya na klabu hiyo ambao utamalizika 2017. Kocha huyo raia wa Chile alijiunga na City akitokea Malaga mwaka 2013 na kuingoza timu hiyo kunyakuwa taji la Ligi Kuu na Kombe la Ligi katika msimu wake wa kwanza. Kulikuwa na taarifa kuwa City wanaangaia uwezekano wa kutafuta kocha mwingine na kuhusishwa na tetesi za kumuwania kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola, hata hivyo taarifa hizo sasa zinabaki kuwa historia baada ya kuthibitika kuwa Pellegrini atanndelea kubakia Etihad. Akihojiwa Pellegrini amesema anajivunia kuinoa City ndio maana amefurahia kusaini mwingine utakaomuwezesha kuendelea kuwepo hapo.
No comments:
Post a Comment