MSHAMBULIAJI nyota wa Manchester City Sergio Aguero anatarajiwa kuukosa mchezo wa ufunguzi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Juventus utakaofanyika kesho katika Uwanja wa Etihad kutokana na majeraha ya goti. Aguero mwenye umri wa miaka 27 alipata maumivu hayo kufuatia kukwatuliwa na Scott Dann juzi katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Crystal Palace. Pamoja na kumkosa Aguero lakini City wamepata habari njema kufuatia winga Raheem Sterling na kiungo David Silva kupona majeruhi yaliyokuwa yakiwasumbua na kuwa fiti kwa ajili ya mchezo huo. Akihojiwa Meneja wa City Manuel Pellegrini amesema Aguero hatakuwa fiti kwa ajili ya mchezo huo lakini ana matumaini atakuwa amepona kwa ajili ya mechi ya ligi dhidi ya West Ham United Jumamosi hii.
No comments:
Post a Comment