KLABU ya Barcelona jana ilipokea kipigo kizito cha kwanza katika La Liga wakiwa chini ya meneja Luis Enrique kufuatia Celta Vigo kutibua rekodi yao ya kutofungwa msimu huu. Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Iago Aspas alifunga mabao mawili baada ya Nolito kufunga bao la kuongoza wakati la mwisho likifungwa na mshambuliaji wa zamani wa Manchester City na Stoke City John Guidetti. Bao la kufutia machozi la Barcelona lilifungwa na Neymar na kuifanya timu hiyo kupoteza mchezo wa kwanza kati ya michezo 25 ya La Liga waliyocheza. Akihojiwa baada ya mchezo huo Enrique amesema kikubwa kilichoamua mchezo huo ni jinsi Celta Vigo walivyocheza kwa umahiri mkubwa kuliko wao. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa walijaribu kutengeneza nafasi lakini walikuwa hawakujipanga vyema kwani wapinzani wao walikuwa bora zaidi yao.
No comments:
Post a Comment