SHIRIKISHO la Soka la Brazil, CBF limekata rufani Mahakama ya Kimataifa ya Michezo-CAS kutaka mechi zilizosalia za kimataifa katika adhabu aliyopewa Neymar kusogezwa mbele mpaka michuano mingine ya Copa Amerika. Mshambuliaji huyo wa Barcelona alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja katika mchezo wa hatua ya makundi ya michuano ya Copa Amerika dhidi ya Colombia Juni mwaka huu. Neymar alipewa kadi hiyo baada ya kumpiga na mpira kwa makusudi Pablo Armero kabla ya kumpiga kichwa Jeison Murillo na kulimwa adhabu ya kutocheza mechi nne za kimataifa. Neymar amebakisha mechi mbili katika adhabu yake hiyo, huku mwenyewe akiwa tayari ameomba radhi kwa tukio hilo.
No comments:
Post a Comment