Friday, September 18, 2015

FA KUMCHUNGUZA MOURINHO.

CHAMA cha Soka cha Uingereza-FA kitafanyia uchunguzi malalamiko kuwa meneja wa Chelsea Jose Mourinho alitumia lugha ya matusi au kijinsia kwa daktari wa timu hiyo Eva Carneiro. Mwananchi mmoja aliwatumia barua pepe FA, ambao wanachaguza picha ya video ya mchezo huo uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Swansea City Agosti 8 mwaka huu. Carneiro hajarejea kazini bado baada ya kukosolewa na Mourinho na kuonekana hawezi kufanya kazi yake kwa ufanisi. Kama Mourinho akikutwa na hatia kuna hatari ya kufungiwa mechi nne kulingana na sheria za adhabu ya makosa kama hayo. Chelsea ambao wanakwaana na Arsenal katika Uwanja wa Stamford Bridge kesho wamekataa kutoa kauli yeyote kuhusiana na masuala ya ndani ya klabu.

No comments:

Post a Comment