BEKI wa Manchester United Luke Shaw amefanyiwa upasuaji wa pili leo katika mguu wake uliovunjika. Shaw yuko katika hospital ya St Anna Ziekenhuis alikopelekwa mara baada ya kuvunjika mguu katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya PSV Eindhoven ya Uholanzi. Nyota huyu aliumizwa na beki Hector Moreno dakika ya 15 ya mchezo, familia ya mchezaji huyo imekwenda Uholanzi kumuangalia chipukizi huyo. Beki huyo kisiki wa upande wa kushoto atakosa sehemu kubwa msimu wa ligi huku akitarajiwa kurejea uwanja tena mwezi Machi mwakani.
No comments:
Post a Comment