Thursday, September 17, 2015

CAMEROON KUFANYA UCHAGUZI BAADA YA RAIS WAKE KUSWEKWA LUPANGO KWA UFISADI.

CAMEROON inatarajiwa kuepuka adhabu ya kufungiwa kimataifa kwa kufanya uchaguzi wake wa kutafuta kiongozi mpya wa Shirikisho la Soka la nchi hiyo-Fecafoot Sepetmba 28 mwaka huu. Uchaguzi wa rais mpya na kamti na wajumbe wa kamati ya utendaji ni lazima ufanyike kwa tarehe hiyo kama Fecafoot wanataka kuepuka adhabu ya kufungiwa iliyotolewa na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA. Msemaji wa kamati ya uchaguzi wa shirikisho hilo, Laurence Fotso amesema mipango yote imeshakamilika na kinachosubiriwa sasa ni uchaguzi huo. Rais wa mwisho kuchaguliwa na Fecafoot, Iya Mohamed anatumikia kifungo jela toka Septemba 3 mwaka huu. Mohammed mwenye umri wa miaka 65 amehukumiwa miaka 15 jela baada ya kukutwa na hatia ya ufisadi katika kampuni ya katani ya Sodecoton na mahakama maalumu ya makosa ya jinai.

No comments:

Post a Comment