KLABU ya Manchester City imepata pigo kufuatia nahodha na beki wake mahiri Vincent Kompany kutolewa nje katika mchezo wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambao walifungwa na Juventus. Kompany aliisaidia City kupata bao la kuongoza katika mchezo huo kwa kumpa shinikizo Giorgio Chiellini mpaka kujifunga mwenyewe. Hata hivyo, alipata majeruhi baadae wakati Juventus wakipambana na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika Uwanja wa Etihad. Meneja wa City Manuel Pellegrini amesema kwasasa wanasubiria kuona vipimo vitasemaje ili kuona ukubwa wa tatizo lake. Kompany mwenye umri wa miaka 29, nafasi yake ilichukuliwa na Nicolas Otamendi aliyenunuliwa na City kwa kitita cha paundi milioni 32.5 kutoka Valencia kiangazi hiki.
No comments:
Post a Comment