MAWAKILI wa Steven Gerrard wamekanusha tuhuma zilizotolewa na El Hadji Diouf kuwa nahodha huyo wa zamani wa Liverpool alikuwa akiwachukia wachezji weusi. Diouf alitoa madai hayo wakati akihojiwa na radio moja nchini Senegal akijibu shutuma zilizotolewa kwake na Gerrard katika kitabu chake ambacho kitatolewa baadae mwezi huu. Nyota huyo wa zamani amesema wakati akiwa Liverpool alimuonyesha Gerrard kuwa yeye mweusi na sio Muingereza jambo ambalo hakuwahi kulifurahia na kufikia hatua hata kushindwa kumtizama machoni. Hata hivyo mawakili wake walikanusha tuhuma hizo wakidai kuwa ni za uongo na zina lengo la kuchafua heshima ya mteja wao aliyojijengea.
No comments:
Post a Comment