MENEJA wa Bayern Munich, Pep Guardiola amemmwagia sifa kemkem Mario Gotze na kukiri kumuelewa uchu wa kiungo huyo kupata muda zaidi wa kucheza. Gotze ameacha katika mechi moja pekee katika Bundesliga msimu huu lakini alifunga bao la pili katika ushindi wa mabao 3-0 waliopata dhidi ya Olympiakos jana baada ya kutajwa katika kikosi cha kwanza kwa ajili ya mchezo huo wa ufunguzi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya. Guardiola amesisitiza hana shaka juu ya uwezo wa kiungo huyo lakini amesema ni vigumu kupata nafasi mbele ya wachezaji wengine waliopo katika kiwango cha juu kama Ronerto Lewandowski na Thomas Muller ambaye alifunga mabao mawili katika mchezo huo. Kocha huyo amesema anampenda Gotze kwani mchezaji wa juu na ana ubora wa hali ya juu lakini tatizo ni kwamba tayari anao kina Lewandowski na Muller. Guardioa aliendelea kudai kuwa anafahamu masikitiko yake lakini yupo pale kwa ajili ya kumsaidia na kumpa nafasi kadri itakavyopatikana.
No comments:
Post a Comment