Wednesday, September 16, 2015

PELLEGRINI AKATAA KUMLAMU STERLING.

MENEJA wa Manchester City, Manuel Pellegrini amekataa kumlamu Raheem Sterling kwa kipindi cha mabao 2-1 nyumbani kutoka kwa Juventus katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya jana. Sterling ambaye alijiunga na City akitokea Liverpool majira ya kiangazi amekuwa katika kiwango kizuri katika Ligi Kuu na kuisaidia timu hiyo kushinda mechi zao zote tano za ligi walichocheza. Lakini Sterling ameingia katika utata baada ya kukosa nafasi mbili za wazi katika mchezo dhidi ya Juventus na baadae kujikuta akitolewa katika dakika ya 71. Akihojiwa Pellegrini amesema hadhani matokeo hayo waliyopata ni kwasababu ya makosa ya yaliyofanywa na Sterling. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa walimiliki mchezo huo vyema na hawakuwa na matatizo mengi ila katika soka mambo kama hayo ni ya kawaida. City watakuwa wakitegemea kupata alama katika mchezo wao unaofuata wa kundi D wakati watakapokwaana na Borussia Monchenglabach Septemba 30 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment