Thursday, September 17, 2015

WENGER ADAI WALIKOSA BAHATI.


MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amedai kuwa kikosi chake kilikosa bahati baada ya kuchakazwa kwa mabao 2-1 na Dinamo Zagreb katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya. Katika mchezo huo Wenger alifanya mabadiliko sita katika kikosi chake baada ya kushinda mchezo wa Jumamosi iliyopita dhidi ya Stoke City. Mshambuliaji nyota Olivier Giroud alitolewa nje kwa kadi nyekundu katika dakika ya 40 ya mchezo na Wenger analaumu kadi hiyo kuwa haikuwa ya lazima. Akihojiwa Wenger amesema anadhani bao la kwanza mchezaji wa Zagreb alikuwa ameotea na kadi iliyotolewa anadhani haikuwa sahihi kwani lilikuwa sio tukio la kudhamiria. Wenger aliwaacha wachezaji wake wa kikosi cha kwanza ambao ni golikipa Petr Cech, beki wa kushoto Nacho Monreal, kiungo Aaron Ramsey na beki wa kulia Hector Bellerin.

No comments:

Post a Comment