WINGA wa Barcelona, Rafinha anatarajiwa kufanyiwa upasuaji baada ya vipimo kuonyesha kuwa alichanika mshipa wa ndani wa goti. Nyota huyo wa kimataifa wa Brazil alikwatuliwa na Rdja Nainggolan wa AS Roma dakika nne baada ya kuingia uwanjani katika Uwanja wa Olimpico kabla ya kutolewa nje kwa kigari maalumu. Mabingwa hao wa Ulaya sasa wamethibitisha kuwa nyota huyo anatarajiwa kufanyiwa upasuaji ili kurekebisha majeruhi hayo. Meneja wa Barcelona Luis Enrique ameeleza masikitiko yake kwa kuumia kwa winga wake huyo huku akidai anadhani inaweza kuwaathiri wachezaji wengine. Enrique amesema kuumia kwa Rafinha kuliathiri mchezo kwa kiasi Fulani kwani wachezaji walipunguza ari.
No comments:
Post a Comment