MIJI ya Los Angeles, Hamburg, Rome, Budapest na Paris inatarajiwa kuchuana kutafuta mwenye wa michuano ya Olimpiki mwaka 2024. Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki-IOC inatarajiwa kuchagua mshindi katika kura zitakazopigwa Septemba mwaka 2017 huko Lima, Peru. Meya wa mji wa Toronto John Tory alitangaza Jumatatu kuwa jiji hilo limeamua kujitoa kutokana na kutingwa na majukumu mengine. Sheria mpya iliyobadilishwa Agosti mwaka huu na IOC inaihakikishia miji yote inayotafuta uenyeji wa michuano hiyo kufuzu mpaka hatua ya mwisho. Sheria hiyo imebadilishwa baada ya miji minne, Oslo, Stockholm, Krakow na Lviv kujitoa katika kinyang’anyiro cha michuano ya olimpiki ya majira ya baridi mwaka 2022.
No comments:
Post a Comment