Wednesday, September 16, 2015

WILSHERE MAJANGA.

KIUNGO wa Arsenal, Jack Wilshere atalazimika kufanyiwa upasuaji katika mguu wake wa kushoto na anategemewa kukaa nje ya uwanja kwa miezi mitatu. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 alivunjika mfupa wa mguu wake wa kushoto Agosti mwaka huu lakini alitegemewa kurejea uwanjani Septemba baada ya mapumziko ya kimataifa. Hata hivyo, klabu hiyo sasa imedai kuwa Wilshere anahitaji kuwekewa kifaa maalumu katika mguu wake hivyo atalazimika kufanyiwa upasuaji. Taarifa hiyo ya klabu iliendelea kudai kuwa kufuatiwa vipimo alivyofanyiwa imeonekana kiungo huyo anapona taratibu sana hivyo inaweza kuchukua hata zaidi ya miezi mitatu. Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amesema Wilshere bado mdogo na anaweza kuvuka kikwazo hicho kigumu na kurejea akiwa imara zaidi.

No comments:

Post a Comment