KATIBU mkuu wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Jerome Valcke amepewa likizo na kusimamishiwa majukumu yake mpaka zitakapotolewa taarifa zaidi. Magazeti jana yalimhusisha Valcke mwenye umri wa miaka 54 na tuhuma za kuuza tiketi za Kombe la Dunia kwa bei ya juu kulinganisha na thamani halisi ya tiketi hizo. Hata hivyo, katibu mkuu huyo raia wa Ufaransa ambaye amekuwa akishikilia wadhifa huo toka mwaka 2007 alikanusha tuhuma hizo. Shirikisho hilo limekuwa likikumbwa na madai mbalimbali ya ufisadi toka Mei mwaka huu wakati maofisa wa polisi walipongia hotelini jijini Zurich na kuwakamata maofisa kadhaa wa juu wa shirikisho hilo.
No comments:
Post a Comment