MAPATO ya klabu ya Manchester United, yameanguka kwa paundi milioni 38 msimu uliopita baada ya kushindwa kufuzu michuno ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Jumla ya mapato ya timu hiyo yamekuwa paundi milioni 395.2 kutoka paundi milioni 433.2 lakini fedha za ufadhili ziliongezeka na kuvunja rekodi kwa asilimia 14 na kufikia pauni milioni 154.9. Hatua hiyo ilisababisha mapato ya watu wanaoingia uwanjani kushuka kwa asilimia 16 na kufikia paundi milioni 90.6 huku mapato ya utangazaji yakishuka na kufikia paundi milioni 107.7 ikiwa ni tofauti ya paundi milioni 28.1. Kutofuzu kwa michuano ya Ulaya kuliigharimu klabu hiyo paundi milioni 35 kupitia mapato ya mechi na yale ya utangazaji.
No comments:
Post a Comment