MENEJA wa Chelsea, Jose Mourinho amekwaruzana na kocha wa Everton Roberto Martinez baada ya kusubirishwa katika mkutano na wanahabari kufuatia kipigo cha mabao 3-1 walichopata katika Uwanja wa Goodison Park Jumamosi iliyopita. Vyombo vya habari vya Uingereza vimeripoti kuwa Mourinho alichukizwa na kuamua kuingilia mazungumzo ya Martinez wakati akizungumza na kundi la wanahabari karibu na uwanja. Taarifa zinadai kuwa akiwa kama meneja wa timu iliyokuwa ugenini, Mourinho alitegemea kuruhusiwa kuzungumza na wanahabari kwanza ili waweze kwenda kujiandaa na safari yao ya kurejea nyumbani. Taarifa hiyo ilimkariri Mourinho akimwambia Martinez kuwa siku nyingine anapaswa kumruhusu yeye kwanza azungumze kabla yake kwasababu wanatakiwa kusafiri. Hata hivyo Martinez alimjibu kuwa hakuwa na mamlaka ya kuwazuia wanahabari kuzungumza naye kwanza. Chelsea wanakabiliwa na kibarua kingine kizito mwishoni mwa wiki hii wakati watakapowakaribisa Arsenal katika Uwanja wa Stamford Bridge.
No comments:
Post a Comment