NAHODHA wa Manchester City, Vincent Kompany amemuonya Kevin De Bruyne kuwa na anapaswa kukubali kwamba sio mara zote atacheza kama namba 10. Nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji aliyevunja rekodi ya usajili wa klabu hiyo kiangazi hiki alitokea benchi na kucheza mechi yake ya kwanza katika ushindi mwembamba wa bao 1-0 iliyopata City dhidi ya Crystal Palace Jumamosi iliyopita. Lakini Kompany amesema De Bruyne akiwa chini ya meneja Manuel Pellegrini anapaswa kujiongeza na kukubali kucheza nafasi zaidi ya moja uwanjani. Nahodha huyo amesema City ina wachezaji wengi ambao wanaweza kucheza nyuma ya mshambuliaji wa mwisho wakiwemo Samir Nasri, David Silva, Raheem Sterling na Jesus Navas. Kompany aliendelea kudai kuwa nafasi hiyo ina wachezaji kama watano ambao wote wana uwezo mkubwa hivyo De Bruyne anapaswa kukubali kucheza nafasi nyingine ili aweze kupata nafasi ya kucheza.
No comments:
Post a Comment