KIUNGO wa Manchester United, Juan Mata amedai kuwa golikipa wa timu hiyo David De Gea haonekani kuathirika kwa chochote pamoja na kipindi kigumu alichopitia katika siku chache zilizopita. Golikipa huyo mwenye umri wa miaka 24 hajaichezea United msimu huu kwasababu ya kuwaniwa na Real Madrid huku dili lake la kwenda huko likishindikana katika dakika za mwisho. Lakini Mata amesema De Gea ambaye amejumuishwa katika kikosi cha United kitakashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, yuko tayari kucheza. Mata amesema De Gea anaonekana yuko kawaida kama alivyokuwa huko hivyo anadhani zile hekaheka za siku chache hazikumuathiri kwa kiasi chochote.
No comments:
Post a Comment