KOCHA wa zamani wa timu ya taifa ya Italia, Cesare Prandelli ana matumaini makubwa kwa Mario Balotelli, akidai kuwa matukio yake tata huko nyuma yamemfanya kupevuka zaidi kufuatia kurejea AC Milan. Balotelli ametengeneza vichwa vya habari kwa miaka kadhaa kutokana na tabia zake na kufanya wadau wengi kuamini nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 hataweza kufikia malengo yaliyotegemewa. Hata hivyo, Prandelli anaamini mchezji huyo sasa anaweza kufikia malengo yake kutokana na kukomaa kiumri na kiakili. Prandelli amesema Balotelli ana moyo mzuri na amekuwa akimhusudu mara zote huku akifurahishwa na kauli aliyotoa wakati akirejea Milan. Kocha huyo amesema kauli ya kuachana na mambo yasiyokuwa na maana yaliyokuwa yakimpotezea muda mwingine ni kauli ya kishujaa na kama akiifuata anaweza kufika mbali zaidi.
No comments:
Post a Comment