Monday, September 7, 2015

ROONEY AWATAKA WACHEZAJI WENZAKE WAIGE MFANO WAKE JINSI BATA LILIVYOMPONZA EURO 2012.

NAHODHA wa timu ya taifa ya Uingereza, Wayne Rooney amewataka wachezaji wenzake wa kikosi hicho kujifunza kutokana na makosa yake aliyofanya katika michuano ya Euro 2012, wakati alipokwenda mapumzikoni na familia yake huko Las Vegas. Uingereza imefuzu michuano ya Euro 2016 na Rooney anaamini wachezaji wenzake wanaweza kunufaika kwa kubakia nyumbani kabla ya michuano hiyo ambayo inatarajiwa kufanyika nchini Ufaransa Juni mwakani. Rooney mwenye umri wa miaka 29, ambaye alisimamishwa kucheza mechi mbili za kwanza za michuano hiyo iliyopita, amesema alikwenda mapumzikoni jambo ambalo analijutia. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa alidhani hakutakuwa na tatizo na sasa anajutia uamuzi wake huo. Rooney amesema kusafiri umbali mrefu hukuchukua muda mrefu pia kuondokana na uchovu na hilo ndio jambo lililomkuta kipindi hicho.

No comments:

Post a Comment