WAENDESHA mashitaka wa Uswisi wamethibitisha kwamba Shirikisho la Soka Duniani-FIFA limekubali kuweka wazi akaunti ya barua pepe mali ya katibu mkuu wa shirikisho Jerome Valcke. Valcke alisimamishwa kibarua chake hicho wiki iliyopita kufuatia madai kwamba alihusika katika mpango wa kuuza tiketi za Kombe la Dunia kwa thamani ya juu. Wanasheria wa Valcke wamekanusha madai ya mteja wao kuhusika katika tukio hilo. Maafisa wa Uswisi wameanzisha uchunguzi wa rushwa sambamba na idara moja ya Haki ya Marekani, ambayo ina washitaki maafisa kumi wa soka kwa tuhuma za rushwa.
No comments:
Post a Comment