MENEJA wa Zenit St. Petersburg, Andre Villas-Boas amesema mipango ya kikosi chake kuwaruhusu Valencia kutawala mchezo ndio iliyowasaidia kupata ushindi wa mabao 3-2 ktika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya uliochezwa jana. Valencia walimiliki mpira kwa asilimia 62 katika mchezo huo huku wakipiga mashuti 15 langoni mwa Zenit ambao wao walipiga saba. Akihojiwa mara baaa ya mchezo huo kocha huyo wa zamani wa Chelsea na Tottenham Hotspurs amesema walicheza vyema ingawa waliwaruhusu Valencia kumiliki sehemu kubwa ya mchezo na huo ndio ulikuwa mpango wao ili wawafunge kwa mipira ya kushtukiza. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa mpango huo ndio uliowasaidia kupata mabao matatu na anadhani walistahili matokeo hayo.
No comments:
Post a Comment