Wednesday, October 7, 2015

BECKENBAUER AMPIGIA DEBE TOKYO SEXWALE KARIKA URAIS FIFA.

NGULI wa zamani wa soka Franz Beckenbauer amemuunga mkono Tokyo Sexwale kama mgombea anayefaa kugombea nafasi ya urais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA na kuongeza kuwa raia huyo wa Afrika Kusini ategemee kuungwa mkono na Shirikisho la Soka la Ujerumani-DFB. Akihojiwa Backenbauer ambaye amewahi kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya FIFA amesema DFB inafahamu uwezo wa Sexwale hivyo hana shaka kuwa watamuunga mkono. Sexwale alikuwa mwanaharakati wa zamani kupinga ubaguzi wa rangi ambaye aliwekwa jela moja na rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela huko Robben Island. Hata hivyo Sexwale mwenye umri wa miaka 62 hajatangaza kama atagombea nafasi hiyo katika uchaguzi utakaofanyika Februari mwakani. Beckenbauer mwenye umri wa miaka 70 alifanya kazi na Sexwale katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2006 iliyofanyika Ujerumani pamoja na ile iliyofanyika nchini Afrika Kusini mwaka 2010.

No comments:

Post a Comment