Friday, October 2, 2015

BOATENG KUFANYA MAZOEZI NA AC MILAN.

KIUNGO wa kimataifa wa Ghana, Kevin-Prince Boateng anatarajiwa kuendelea kufanya mazoezi na klabu yake ya zamani ya AC Milan wakati akitafuta timu mpya baada ya kufungiwa na Schalke. Schalke walimsimamisha Boateng Mei mwaka huu baada ya kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Cologne, sababu kubwa ikiwa ni kutoaminiana kati ya klabu na mchezaji huyo. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28 alikuwa akitarajiwa kujiunga na Sporting Lisbon kipindi hiki cha kiangazi lakini taarifa zilidai kuwa alishindwa kufaulu vipimo vya afya. Sasa Boateng anatarajia kufanya mazoezi na Milan klabu ambayo ndio aliyotoka kwenda Schalke, mpaka Desemba 31.

No comments:

Post a Comment