MSHAMBULIAJI wa Manchester City, Wilfried Bony amebainisha kupata maradhi ya malaria mapema mwaka huu. Bony alishindwa kusafiri katika ziara ya City yakujianda na msimu walizokwenda Australia na Vietnam kwasababu ya maradhi hayo. City hawakutoa taarifa kamili ya sababu za kukosekana kwa Bony kipindi hicho zaidi ya kusema kuwa mshambuliaji huyo wa zamani wa Swansea City alikuwa akiumwa. Lakini baada ya meneja wa City Manuel Pellegrini kutaja katika mkutano na wanahabari wiki hii kuwa alizungumza na Bony kuhusu majeruhi yaliyokuwa yakimsumbua na maradhi, nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 amekiri kuugua ugonjwa huo. Akizungumza mara baada ya mchezo dhidi ya Bournemouth walioshinda mabao 5-1 huku yeye akifunga mawili, Bony amesema alipata malaria kutoka Afrika wakati akirejea lakini sasa hivi yuko sawa.
No comments:
Post a Comment