MSHAURI wa zamani wa rais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Sepp Blatter, Jerome Champagne amesema anafikiria kuwania nafasi hiyo katika uchaguzi ujao. Champagne alijaribu kushindana na Blatter katika uchaguzi uliofanyika Mei mwaka huu lakini alishindwa kupata watu kumuunga mkono ili ateuliwe. Kusimamishwa kwa Blatter na rais wa Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA Michel Platini kupisha uchunguzi wa malipo ya euro milioni 1.35, kunamsukuma Champagne kutaka kujaribu tena kugombea nafasi hiyo. Champagne ametangaza kuwa kama akichaguliwa wakati atakapogombea ataweka wazi mishahara na marupurupu ya maofisa wa shirikisho hilo. Champagne sasa anaungana na Prince Ali bin al-Hussein wa Jordan, mchezaji wa zamani wa Trinidad na Tobago David Nakhid na rais wa Shirikisho la Soka la Asia, Sheikh Salman bin Ebrahim Al Khalifa ambao tayari wametangaza nia ya kugombea.
No comments:
Post a Comment